Ut tellus dolor, dapibus eget, elementum ifend cursus eleifend, elit. Aenea ifen dn tor wisi Aliquam er at volutpat. Dui ac tui end cursus eleifendrpis.
Simu Namba:
+255736932424
S. L. P. 30852 Kibaha, Pwani
Tanzania
Barua Pepe:
info@nyumbusaccos.co.tz
NYUMBU Savings and Credit Cooperative society Limited (NYUMBU SACCOS LTD) ilianzishwa na kuandikishwa tarehe 18/09/1989 na kupewa Hati ya usajili namaba CR 290 kwa sheria ya ushirika ya mwaka 1982 ambapo kwa sasa Chama kinafanya shughuli zake chini ya Sheria namba 6 ya Ushirika ya mwaka 2013 na kanuni zake sambamba na Sheria ya Taasisi ndogo za Fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019.
DIRA
Dira yetu ni kuwa moja ya SACCOS bora zinazotoa huduma bora kwa wanachama wake katika Tanzania (Kama ilivyo katika Mpango Mkakati wa NYUMBU SACCOS LTD)
DHIMA
Dhima kuu ya NYUMBU SACCOS LTD ni kutoa huduma za akiba na mikopo kwa wanachama wake pamoja na kuinua na kustawisha hali ya uchumi na maisha yao kwa kuanzisha na kumiliki -NYUMBU SACCOS kidemokrasia na kuchangia mtaji na kukubali kuyakabili matatizo na kupata manufaa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika.
NYUMBU SACCOS LTD inatoa aina mbalimbali za bidhaa na huduma zilizoundwa ili kukidhi mahitaji mahususi ya wanachama wetu. Bidhaa na huduma zetu ni pamoja na:-
Tunalenga kutoa masuluhisho ya hali ya juu ambayo yanaendesha mafanikio ya wanachama na kuzidi matarajio yao.
Bodi inao wajibu wa kusimamia shughuli za NYUMBU SACCOS LTD ikishirikiana na Kamati ya Usimamizi, Kamati ya Mikopo na Menejimenti kuhakikisha kuwa inatambua maeneo yenye athari kwa shughuli, ,kupanga, kuamua na kusimamia shughuli za uwekezaji, mambo muhimu ya fedha, kupitia na kufanya tathmini za bajeti pamoja na mpango mkakati. Bodi inalo jukumu pia la kuhakikisha kuwa mfumo wa udhibiti wa ndani pamoja na sera madhubuti zinakuwepo na zinafuatwa kwa kuzingatia kanuni na misingi ya utawala bora.
Kulingana na Katiba ya NYUMBU SACCOS LTD, Bodi inapaswa kukutana angalau mara nne kwa mwaka. Bodi imekasimu shughuli za kila siku za kiutendaji wa NYUMBU SACCOS LTD kwa Meneja. Meneja ndiye katibu wa vikao vya Bodi na Mkutano Mkuu pia ni kiungo kati ya menejimenti ya NYUMBU SACCOS LTD na Bodi.
NYUMBU SACCOS LTD inaendeshwa kwa kufuata misingi na kanuni ya utawala bora. Wajumbe wa Bodi wanatambua umuhimu wa uadilifu, uwazi na uwajibikaji. Kamati za Bodi zipo tatu (3) ambazo ni kamati ya mikopo, Kamati ya elimu na Kamati Tendaji.